Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Koffi Olomide atuma ujumbe kwa Wakenya

Koffi Kenya(1) Koffi Olomide atuma ujumbe kwa Wakenya

Thu, 14 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wiki moja baada ya kuoneshwa mapenzi ya kweli na mashabiki wake wa Kenya, gwiji wa Rhumba Koffi Olomide angali bado kuamini haiba ya juu ya makaribisho aliyopokezwa na mashabiki wake.

Kupitia kurasa zake mitandaoni, Olomide alishiriki video fupi akitoa shukrani zake kwa mashabiki na kuonesha ni jinsi gani maneno hayawezi kutoshea kuashiria ni jinsi gani alifurahi kwa mapokezi na mbwembwe za mashabiki katika muda wa saa mbili na sekunde 35 alizotumbuiza jukwaani katika uwanja wa ASK Dome, Ngong Road mnamo Jumamosi Desemba 9.

Olomide alisema kwamba mashabiki wake wa Kenya walimpa nguvu ya kujiamini baada ya miaka 6 ya kutopata nafasi ya kutua nchini na kuwataja kama mashabiki wa kupigiwa mfano chanya kote duniani.

“Mashabiki wangu wapendwa, mashabiki wangu wa Kenya, familia yangu pendwa, kabla niondoke Nairobi ningependa kusema ahsante, ningependa muipokee shukrani yangu kwa ukamilifu kwa kuwaona tena mlijitokeza kwa wingi katika shoo miaka sita baadae. Mlinifanya kujihisi mwanamume mwenye furaha…”

“Ninajihisi mwenye nguvu na jukumu langu kuanzia sasa ni kustahiki ujasiri wenu tena na tena na urafiki wenu. Mbarikiweni sana, nyinyi ni mashabiki wazuri Zaidi katika dunia hii, ninajivunia uwepo wenu. Ombi langu ni kurudi tena kutembelea majiji ya Kenya, Eldoret, Kisumu, Mombasa… hadi nasahau majina… mbarikiwe sana, sisi sote ni familia. Ahsante, ahsante sana kutoka ndani ya moyo wangu,” alimaliza Olomide.

Olomide aliwapunga mashabiki wake kwa densi za kukata na shoka huku akiwa amevalia viatu yenye visigino virefu na kuonesha umahiri wake wa kucheza navyo jukwaani kwa Zaidi ya saa mbili licha ya umri wake kuzidi.

Shoo hiyo – Peace Concert – iliandaliwa na kufahdiliwa na shirika la habari la Radio Africa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live