Dar es Salaam. Mwanamuziki kutoka Jamuhuri ya Demokrasia ya Kongo, Koffie Olomide ameeleza mpango wake wa kuingia studio kurekodi wimbo na msanii Nandy. Koffie ameyasema hayo leo Ijumaa Machi 6, 2020 katika mahojiano na kituo cha redio Clouds, yaliyolenga kuzungumzia onyesho lake litakalofanyika kesho ukumbi wa Mlimani City. Katika mahojiano hayo, Koffie pamoja na mambo mengine amtaja mwanamuziki ambaye anampenda nchini Tanzania kuwa ni Nandy huku akibainisha wimbo wake unaomkosha ni 'Kivuruge'. "Nampenda sana Nandy na wimbo wake wa Kivuruge ambapo kila nikiusikiliza nasikia raha, kama mnayo niwekeeni," ameagiza Koffie na kupigia wimbo huo ulimfanya kucheza akiwa kwenye kiti. Pia amebainisha kuwa licha ya kumfatilia msanii huyo anayetesa na wimbo wa "'Na nusu' kwa sasa, kwa mara ya kwanza wamekutana naye leo na tayari wameongea mipango ya kufanya naye kazi ambapo karibuni wataingia studio. studio .