Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kodi anayolipa Diamond Platnumz kwa mwaka

Diamond Cheni. Kodi anayolipa Diamond Platnumz kwa mwaka

Tue, 7 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Staa wa muziki Tanzania na Africa kwa ujumla Diamond Platnumz ameweka wazi kiasi cha kodi anacholipa kwa mwaka ambapo ni Tsh Bilioni 1.7.

Diamond ameeleza hilo kwenye mkutano wa Zoom ambao umekutanisha wadau wa siasa na viongozi mbali mbali kuelekea miaka 60 ya Uhuru.

"Serikali imetengeneza mazingira rafiki kurasimisha tasnia ya muziki na kuiwekea wepesi kwenda kwenye sekta rasmi, mfano mimi kutoka kwenye uwanamuziki mpaka nimekuwa mkurugenzi wa makampuni mbalimbali" 

"Nilikuwa nafanya mahesabu hapa namna ya kimapato huu mwaka kwa kodi ambazo tumezichangia ni Bilioni 1.7, najivunia Serikali imeniwekea mifumo sahihi najiona ni mlipa kodi na nachangia kwa namna moja au nyingine".  

Chanzo: www.tanzaniaweb.live