China imezindua Kliniki mpya katika Hospitali ya Watoto ya Shanghai ambayo itahusika kusaidia Watoto wanaokumbana na changamoto katika somo la hisabati ambapo tayari Kliniki hiyo iitwayo ‘Spatial and Mathematical Learning Difficulties Clinic’ imeanza kutoa huduma zake rasmi October 8 2024, mtandao wa WION umeripoti.
Tafiti zilizofanywa na Wataalam nchini humo, zinaonyesha kuwa Watoto wengi wanaoshindwa na masuala ya geometri wanakabiliwa na namna duni katika sehemu fulani ya ubongo hivyo Kliniki hii itatoa matibabu ya kina kwa Wanafunzi hao ikiwa ni pamoja na ushauri na nafasi ya kujadili matatizo yao kwenye mitandao ya kijamii ili kubaini chanzo.
Kliniki hiyo kila siku ya Jumanne itakuwa ikifanya matibabu hayo na itatoza ada ya yuan 316 (sawa na 120,000/= Tzs) kwa kila Mgonjwa ambapo haitokuwa na kikomo cha umri
Waalimu wa hisabati nchini humo wamepokea vizuri ujio wa Kliniki hiyo japo wengine wamesisitiza kuwa kuna tofauti kati ya ugumu wa kujifunza na matatizo ya kiafya kwani sababu nyingi za kushindwa zinaweza kuwa zinatokana na mbinu zisizofaa na ufundishaji duni.