Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kisa uwekezaji, Wakazi amvaa tena Diamond

Diamond Wakazi Nk Kisa uwekezaji, Wakazi amvaa tena Diamond

Thu, 18 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Usiku wa launchini ya albamu ya msanii Barnaba inayokwenda kwa jina la Love Sound Different usiku wa Agosti 16, 2022, CEO wa Lebo ya WCB, Diamond Platnumz alidai kuwa mazingira na sheria za Tanzania zinawashinda wawekezaji wengi kutoka nje na ndani ya nchi kuwekeza katika tasnia ya muziki Tanzania.

Diamond aliongeza kuwa sheria na kanuni hizo zinazosimamiwa na BASATA na COSOTA zinawabana wawekezaji kiasi kwamba wanakimbia kuwekeza katika tasnia hiyo huku akiishauri Serikali kulegeza sheria hizo ili wawekezaji wengi wavutiwe na iwe rahisi kwa wasanii kupata sapoti kwani Tanzania ina wasanii wengi wenye vipaji lakini tatizo ni sheria ngumu kwa wawekezaji hao.

Diamond aliongeza kuwa anachokifanya sio kuwasapoti wasanii katika lebo yake bali ni biashara kwa hiyo ni lazima kuwe na makubaliano ya kibiashara na lazima yazingatiwe ili mwekezaji na msanii wote kwa pamoja wanufaike.

"Mhe Spika, msanii anapowekezewa pesa, hawi mtu tu wa kawaida, anakuwa brand na anakuwa biashara. Tatizo letu wasanii tukishafika kwenye kilele na pesa zikaanza kuingia msanii anataka zile pesa ale peke yake.

Atatafuta kila namna ya kumkimbia mwekezaji, atamtafutia kashfa, dhulma, mwizi, tapeli. Wanakimbia kujificha kwenye vivuli vya mawaziri, wanasema wanaonewa. Madhara yake ni kwamba wawekezaji wengine wanaogopa kwa sababu sheria haziwasaidii, haziwalindi," amesema Diamond.

Sasa kupitia katika ukurasa wake wa Instagram, Msanii wa Hip Hop, Wakazi amemvaa Diamond na kumhoji iwapo kauli yake hiyo aliyoitoa katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar alikuwa anawasemea BASATA kwa mgeni rasmi ambaye alikuwa Spika wa Bunge la Tanzania, Dkt. Tulia Ackson.

"So Diamond kwenye speech yake alikuwa anawasemea BASATA kwa Spika Tulia au… sijaelewa. It looks like the ruling of the arbitration (Rayvanny) wasn’t in his favor so he mad at them.”

Haya yanakuja huku kukiwa na vuguvugu la kimkataba baada ya msanii Rayvanny kuondoka ndani ya lebo ya WCB na maneno kusambaa kuwa Diamond anawanyonya wasanii wake kimaslahi.

Wiki chache baadaye Diamond na msanii wake huyo wakaonekana katika viunga vya BASATA huku chanzo kikidaiwa kuwa walikuwa na mazungumzo ya kumalizana ili Rayvanny awe huru, lakini pande zote mbili hazijatolea ufafanuzi kuhusu jambo hilo mpaka sasa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live