Mwanasoka kutoka nchini Brazil, NeymarJr na mpenzi wake, Bruna Biancardi wanadaiwa wametengana mwezi mmoja baada ya kupata mtoto wao wa kwanza.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari mbalimbali inaelezwa kuwa uamuzi wao wa kutengana umekuja baada ya tetesi kuwa mchezaji huyo hakuwa muaminifu kwa mpenzi wake.
Biancardi mwenye umri wa miaka 29, inadaiwa kuwa amethibitisha kutokuwa kwenye mahusiano na nyota huyo na wamebaki kuwa wazazi wa mtoto.
Hata hiyo kuna ripoti zinadai kuwa wawili hao walikuwa na mkataba ambao ulimruhusu #Neymar kutaniana na kulala na wanawake wengine kwa masharti maalumu ya mkataba ikiwa ni pamoja na Mbrazili huyo hakuruhusiwa kuwabusu wanawake mdomoni na atalazimika kutumia kinga wakati wa kujamiiana.