Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kisa kunyimwa sh laki 1, Mwijaku awalipua Paula na Kajala

Mwijaku Marioo Kisa kunyimwa sh laki 1, Mwijaku awalipua Paula na Kajala

Wed, 26 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtangazaji wa Clouds FM, Burton Mwenda 'Mwijaku' amewatema nyongo Paula na Kajala kisha kumkumbusha Marioo kwamba asipokuwa makini atafilisika kutokana na tabia yake ya kuwapa pesa mpenzi wake Paula pamoja na mama yake ambaye ni Kajala.

Mwijaku amesema kwa muda mchache aliokaa karibu na Marioo amegundua anatumia pesa nyingi sana kuwafurahisha Paula na Kajala huku ndugu zake akiwaacha solemba.

Mwijaku amesema starehe zote anazofanya Kajala na hata Paula, pesa zinatoka kwa Marioo hata hii sherehe ya Birthday ya Kajala iliyofanyika hivi karibuni gharama yote ilitoka kwa Marioo.

Mwijaku amesema kuna siku alimuomba Marioo laki moja tu, lakini hakupata pesa hiyo aliishia kupigwa tarehe lakini alishangaa kuona Paula anamtunza mama yake mamilioni aliyopewa na Marioo wakati yeye alinyimwa laki moja tu.

"Wote tunafahamu kama Kajala hana kazi yoyote hapa mjini lakini kila siku anakula bata, pesa anatoa wapi? vilevile Paula alishafunga duka lake muda mrefu baada ya sponsa kukataa kulipa kodi, lakini kutwa kula bata.

"Anasuka nywele za gharama kila siku pesa anatoa wapi? wameungana kumfilisi Marioo na asipokuwa makini ndani ya miaka mitatu tutamsahau atabaki anamiliki sauti tu," amesema Mwijaku.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live