Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kisa kumwomba msamaha Diamond, Nay asema “Dulla Makabila hajielewi”

MAKABILA NAY Kisa kumwomba msamaha Diamond, Nay asema “Dulla Makabila hajielewi”

Fri, 17 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rapa nguli wa Bongo, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ ametumia uwanja wake wa Insta story kumchana msanii wa singeli Dulla Makabila kufuatia mkeka aliouandika akimuomba msamaha Diamond Platnumz ili amrejeshe tena kwenye familia ya Wasafi.

Kupitia Insta Stori yake, Nay amedai kuwa baadhi ya wasanii wa Singeli akiwemo Dulla Makabila hawajielewi na kwamba, Makabila ni zero kichwani hivyo anakwenda kaumaliza rasmi mwendo wake kwenye tasnia ya muziki.

"Wasanii wengi wa singeli hawajielewi, kufuatana na mazingira wanayotokea kwenye usela mwingi, no shule hata kidogo ni wachache sana wapo smart, ila #Dullamakabila ni namba moja katika wasiojielewa yani kichwa 0, na leo amemaliza mwendo wake rasmi,'' ameandika Nay.

Kabla ya msamaha wa Dullah, Kama unakumbuka miezi michache nyuma, Dullah Makabila alikuwa yuko karibu na upande wa E Media na kuanza kuuponda upande wa pili (Wasafi Media) akiwemo CEO wa Wasafi Media, Diamond Platnumz kuwa walimtumia kujinufaisha wenyewe wakati Makabila akiendelea kuwa chini kila siku na wanamchafua kisa tu yupo karibu na Majizzo, na anafuraha kuhamia E Media kwa waswahili na muziki wa singeli uliko zaliwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live