Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kisa Kumchamba Wema Kupanda Uber, Aristote Yamkuta Mazito

Aristoteed Kisa Kumchamba Wema, Aristote Yamkuta Mazito

Mon, 31 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MAMBO yametaradadi..... Hivyo ndiyo unavyoweza kusema baada ya mdau wa masuala ya sanaa, Aristote kumwangukia malkia wa Bongo Foeva, Wema Sepetu na kumuomba msamaha baada ya kumkandia kuwa Wema kwa sasa hana pesa anadandia Uber na Bolt tofauti na Irene Uwoya ambaye anatembelea Range.

Katika mahojiano yake na moja ya chombo cha habari, Aristote alidai kuwa Uwoya ni mzuri kimuomekano kuliko Wema jambo ambalo limeibua hisia kwa wadau wa sanaa na mastaa mbalimbali wakitaka Aristote awajibishwe na vyombo vya sheria kitokana na kauli yake hiyo ya udhalilishaji kwa Wema.

Wema Sepetu afunguka mazito; "Wacha nikuweke kabisa kwa page yangu upate kufurahi... maana nimekaa sana mdomoni mwako.... Kutwa huishi kunitaja....

"Kurequest nako ni K vile vile maana nakutanaga na mashabiki pia nikiwa kwenye Uber na Bolt... And by the way, miaka miwili sasa sina gari na mbona maisha fresh tu... Mkitembelea nyinyi ma Range inatosha Aristotee... Sio mbaya....????????????????????????

"Ila ifike muda mnipumzishe basi maana Im nat in a competition na mtu yoyote in my life... Niko na deal na Wema wangu tu... Sijawahi kushindana na mtu... Always stood on my own.... Nashkuru..."

Kwa upande wake Uwoya amejibu; " Nimeona niongee, na nataka niliweke hili wazi na kila mtu aelewe since najikuta nahusishwa kutokana na ukaribu wangu na Aristote, Binafsi Nimesikitishwa sana na maneno yasiyo ya kibinaadamu yaliyotolewa na Aristote dhidi ya Wema.

"Watu waelewe kitu kimoja leo, Sijawahi kumtuma Aristote amtukane Wema wala mtu yeyote yule, sina ugomvi na Wema na sina sababu ya kufanya upuuzi wa namna hiyo, Nimempigia pia Aristote kuoneshwa kukasirishwa kwangu, na niseme tu hiyo ni MIHEMKO yake yeye, sihusiki na lolote juu ya hayo aliyoyaropoka ambayo yanaleta hata uchonganishi baina yetu kitu ambacho sikifurahii kwakweli.

"Kingine nichukue nafasi hii kukupa Pole Wema kwa haya yaliyotokea, hata mimi ningekuwa wewe ningejiskia kama unavyojiskia, pole sana sana, na zaidi Aristote nathamini upendo wako kwangu lakini ningeheshimu sana kama itabaki sisi na maisha yetu bila kunilinganisha wala kunishindanisha na yeyote yule sababu mimi naishi maisha yangu siko kwenye mashindano na mtu, asanteni wote, One love!!"

Jokate naye aibuka; "Ifike muda sheria ifuate mkondo wake kukomesha tabia na hulka za aina hii kwenye jamii zetu. Iwe funzo kwa wote. Na msamaha pekee yake hautoshi. Watu wanajiua kwa kuwa bullied online. This has to stop!!! I believe you will do the necessary @wemasepetu @bestizzo @martinkadindaofficial"

Hamisa Mobetto naye yumo; "Unaboa sana na una kera ufike mahala ufanye maisha yako .... Kama unavyompenda na kumuheshimu mama ako, Mkeo na wanawake wengine katika maisha yako .... Basi na wanawake wengine wasokuhusu wanastahili heshima ya hiyo hiyo.

"Na uache kila mtu aishi anavyotaka yeye na sio wewe. Na Jifunze kusifia ukipendacho bila kukandia vingine .

Dunia ina nafasi kubwa sana ya kila mtu kung'ara.

Msami Baby hajabaki nyuma; "Pole Wema Sepetu mimi nina mtoto wa kike huwa nawaza sana future yake , nimejisikia vibaya sana kuona ile clip yako ya live, watu wanaozunguka wasanii huwa wagombanishi sana kwa kutafuta maslai yao.

"Umaarufu pia kwa watu wasio na talanta kwa miaka hii umepelekea kuibuka kwa talanta ya walopokaji na sio mbaya kwao kwa kuwa wanapata pesa kupitia hiyo kulopoka , lakini jamii haijifunzi kitu kutoka kwao, mbaya zaidi wanatumia nguvu sana kutafuta maudhui kiasi kutumia majina ya watu wengine mpaka kuwaumiza SIO POA.

Aristotee amuomba radhi wema; @wemasepetu Samahani sana my sister ???????????????????? 

Miriam Odemba naye alipuka; "Mnaboa Sana nyie tukiwaomba mpost vitu vya Jamii mnatuweka pembeni lakini kiki za ujinga ndio number one please badilika @aristotee mbona wewe ni mkaka mzuri sana please kuwa na maneno yakuongea kwenye jokes."

View this post on Instagram

A post shared by Tanzania Web (@tanzaniaweb)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live