Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kipini puani, urembo unaovutia na kukera wengi

F  AXJTXMAAulhl Kipini puani, urembo unaovutia na kukera wengi

Wed, 27 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Moja kati ya urembo unaopendwa saana na wanawake, haswa wa mjini mjini ni kipini cha puani. Lakini pia ndiyo urembo ambao unakera wanaume wengi na hata baadhi ya wanawake. Kimsingi ni kaurembo ambako hakana mashiko ya moja kwa moja.

Kautafiti flani hivi 'ameizing' ambako hakana mamlaka kamili ya utafiti, kanaonesha kuwa idadi ya watu wanaopenda kipini cha puani ni ndogo ukilinganisha na wale wanaokerwa lakini hawawezi kusema hadharani.

Kwa lugha nyepesi na laini ni kwamba, urembo wa kipini cha puani ni kama chumvi inapendwa na kuchukiwa 'ati ze semu taimu'. Hata wenye vipini hivyo ukiwauliza kama kweli walivutiwa na urembo huo, hawana jibu la moja kwa moja.

Tunakupa 'homu weki' ukikutana na mwenye kipini muulize alivutiwa na nini'?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live