Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kingwendu aibua jipya "Serikali ituwekee Madaktari wetu"

Kingwendu 1 Kingwendu aibua jipya "Serikali ituwekee Madaktari wetu"

Thu, 17 Dec 2020 Chanzo: millardayo.com

Kufuatia kifo cha muigizaji Mohamedi Fungafunga maarufu kama Mzee Jengua, mchekeshaji Kingwendu amesema anaiomba Serikali iwaangalie wasanii ili wawe na madaktari wao wa kuwafanyia ‘check up’ ya mwili.

Kingwendu amesema suala hilo lingekuwa jema sana kwa wasanii ili wakiumwa wanajua kabisa ni ugonjwa gani ambao unamsumbua pia huepusha utata unaotokeaga kuhusu chanzo cha ugonjwa uliopelekea kifo cha msanii.

“Fundisho kubwa kwa wasanii kama unaumwa usilazimishe kufanya kazi jaribu kufuatilia vipimo hospitalini ili kuangalia afya zetu, pia tungejaribu kuongea na Serikali ituangalie na tuwe na madaktari wetu wa kutufanyia ‘check up’ ili mtu anapoumwa ijulikane anaumwa nini” Kingwendu 

HUZUNI YATAWALA MSIBA WA MZEE JENGUA MASTAA WAJITOKEZA KUMZIKA, KINGWENDU NA STEVE NYERERE WAFUNGUKA

Chanzo: millardayo.com