Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kinasa Msukuma afunguka kushushwa stejini na baunsa wa Diamond

Kinasa Brnaba Diamond.jpeg Kinasa Msukuma afunguka kushushwa stejini na baunsa wa Diamond

Thu, 18 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Usiku wa Jumanne, Agosti 16, 2022 katika Ukumbi wa Mlimani City kulifanyika uzinduzi wa albamu ya msanii mkongwe katika tasnia ya muziki, Barnaba Classic.

Moja ya tukio liliyozua gumzo ni lile la Kinasa Msukuma ambaye alikuwa akiwatunza fedha nyingi Diamond Platnumz na Barnaba wakiwa wanapafomu stejini ambapo alishushwa na baunsa wa Diamond muda mchache baada ya kuanza kufanya hivyo.

Kinasa ameonyesha kusikitishwa na kitendo hicho cha kushushwa stejini tena kwa nguvu wakati akitunza pesa kwani alipanda pale baada ya kutajwa mara kadhaa na Barnaba ambaye amedai kuwa ni ndugu yake na alimtaja jina ili aende kutoa sapoti.

Kinasa amesema kutokana na heshima aliyo nayo kwa Barnaba, ndio maana msanii huyo alikwenda kumfokea baunsa wa Diamond baada ya kumshusha stejini.

“Suala hilo tumeshalimaliza kama wanafamilia wa WCB. Jana nilipokea simu kutoka kwa mwanafamilia na mume wa mama Diamond, Anko Shamte akinishukuru kwa sapoti ninayoionesha kwao na kuniomba tuyamalize yale yote yaliyojitokeza pale Mlimani City wakati wa uzinduzi kwani sisi ni wanafamilia na hakuna haja ya kutofautiana," amesema Kinasa.

Aidha tajiri huyo kijana ameelezea matamanio yake ya kusaidia kina mama wajane na wale wanaoishi kwenye mazingira magumu kwa kuwa anaona ni kundi lililosahaulika katika jamii na linahitaji msaada na amepanga kufanya yote mara baada ya kumaliza kufungua Kampuni yake ambayo ipo kwenye hatua za mwisho kukamilika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live