Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kimeumana Mwijaku na Shilole: Nitaaanika uchafu wako

Shilole162904 Kimeumana Mwijaku na Shilole: Nitaaanika uchafu wako

Wed, 30 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwenye social media kumewaka moto unaambiwa, hii ni baada ya Mwijaku kutoleana povu na kuchambana vilivyo Malkia wa Taarabu Bongo, Hadija Kopa kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii.

Timbwili hilo limemuibua msanii wa Bongo Fleva na mjasiriamali, Shilole ambaye amempost Hadija Kopa 'Mama Zuchu' na kuandika ujumbe huu.

"Mama Khadija ni mwanamuziki ambae mimi nimeanza kumsikia toka mdogo kwetu Igunga mpaka leo mimi ni msanii. Ni mama ambae sisi wanamuziki wa kike tuna muangalia na kutamani uwezo alionao Toka msichana mpaka leo mama na wajukuu.

"Kiukweli unapomkosea heshima huyu mama ni sawa na kutukosea heshima wanawake na sio wanawake tu bali hata mila na tamaduni zetu zimetuasa kuheshimu wakubwa. Sijapenda ulichofanya ndugu yangu Mwijaku naomba umuombe radhi mama Khadija Kopa," amesema Shilole.

Shughuli haikuishia hapo tu, baada ya kauli hiyo, Mwijaku amemvaa Shishi na kumwambia haya kupitia insta story yake akisema;

"Shishi tafadhali sana usinilazimishe niyaseme mauchafu yako. Mwisho mkagombana na mumeo unajua kua naongea uongo kwa mumeo kila anapotaka kujua habari zako.

"Tafadhali nakuheshimu basi niheshimu usinitaje kwenye mambo ya kipuuuzi. Nimekaa na wewe siku saba nimejua tabia zako zoote tuheshimiane tafadhali," amesema Mwijaku.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live