Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kim Kardashian apondwa kisa kujipunguza mwili

Kim K.jpeg Kim Kardashian

Thu, 5 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanadada muigizaji kutokea Marekani Lili Pauline Reinhart amemkejeli mwanamitindo Kim Kardashian kuhusiana na kupungua kwa ajili ya onyesho la Met Gala 2022 lililofanyika usiku wa Mei 2,2022.

Kupitia ukurasa wake wa intagram Lili Reinhart aliandika; "Unafaya mahojiano na unatamba kabisa kuwa ulipunguza kula ili upoteze uzito kwa ajili ya onyesho la Met Gala!?? ili upendeze zaidi na gaunilako!??" alisema Reinhart.

Reinhart aliendelea kwa kusema "Unajua kabisa kuna vijana wengi ambao wanakutazama na unawahamasisha kwa kila unachokifanya alafu unakuja kuwaambia uliacha kula kwa ajili ya onyeshola usiku moja!? inashangaza kweli ujinga umetawala," Lili Reinhart.

Ikumbukwe Kim Kardashian aliliambia jarida la Vogue kuwa ilimpasa kupunguza baadhi ya vyakula ili aweze kupunguza uzito ili aweze kudumisha muonekano mzuri katika onyesho la Met Gala 2022.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live