Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kim Kardashian aguswa na vita ya Israel na Palestine

Kim Kardashian May 2023 Kim Kardashian aguswa na vita ya Israel na Palestine

Thu, 12 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baadhi ya ma-star kutoka nchini Marekani wameonekana kuguswa na vita inayoendelea kati ya #Israel na #Palestina huku baadhi yao wakiungua mkono nchi ya Israel, huku kwa upande wa mwanamitindo maarufu #KimKardashian, yeye hana upande ila amesikitishwa baada ya kuona watoto wachanga na familia zisizo na hatia zinavyoteseka.

Kim kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika ujumbe kwa mara ya kwanza toka vita hiyo itokee, ujumbe wa kuwafariji uliokuwa ukieleza kuwa anawapenda sana marafiki na familia yake ya kiyahudi anawaunga mkono huku akiwatia moyo kuwa wajue hawako peke yao.

Huku akiendelea kwa kuwataka watu wanaochagua upande fulani wawe na mioyo yenye huruma kwa watoto na familia zisizo na hatia bila ya kuangalia wako upande gani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live