Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kim, Kanye Waachana Rasmi, Tena Hadharani

Kanye Kawaka.png Kim, Kanye Waachana Rasmi, Tena Hadharani

Sat, 5 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya Kim Kardashian kumjibu Kanye kuhusu madai ya kufanya vitendo vinavyoweza kumharibu binti yake, kutokana na kumuunganisha mtoto huyo kwenye mtandao wa TikTok, Hatimaye rapa huyo amejibu mapigo kwa kumuandikia ujumbe mwingine kukosoa vikali alichokiandika Kim kuhusu malezi ya mtoto wao.

"Unamaanisha nini unaposema mtoa huduma mkuu? America iliona ulivyojaribu kumficha binti yangu kwenye siku yake ya kuzaliwa kwa kutokutoa anwani ya inapofanyika shughuli, Uliniwekea ulinzi ndani ya nyumba ili kucheza na mwanangu.

Kisha kunishtaki kuwa niliiba, ilibidi nipime dawa za kulevya baada ya sherehe ya Chicago na ulinishtaki kwa madai kuwa natumia dawa za kulevya, Tracy Romulus acha kumdanganya Kim hadi amekuwa namna hii."

Ameandika Kanye kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram. Majibizano ya wawili hao yameanza kupamba moto baada ya Kim kutumia mitandao yake ya kijamii kujibu madai ya Kanye West kuwa hakushirikishwa wakati mtoto wao wa kwanza North West alipounganishwa kwenye mtandao maarufu wa TikTok.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live