Msanii wa zamani wa Lebo ya Konde Music Worldwide, Khalil Tatem maarufu kama Killy amemlipua aliyekuwa bosi wake Harmonize akidai kuwa lebo hiyo haijawahi kumsaidia chochote badala ya kuwanyonya wasanii wake.
Killy amesema hayo mara baada ya Harmonize kufanya mahojiano na kudai kuwa alikuwa akiwasaidia wasanii hao lakini walimtia hasara na kuwataka watafute kampuni nyingine ya kuwasimamia.
"Kwanza kabisa usingeweza kutulipisha hata sumni kwasababu wewe ndiye uliyevunja mkataba hiyo ingekuwa vichekesho na kali ya mwaka zaidi na zaidi wewe ndio tulitakiwa tukulipishe yani utulipe.
"Mfano tungesema twende Mahakamani alafu sheria ifatwe, bro ivi unafikiri ungechomoka, ila sisi watoto wa mjini tukasema tufunike kombe mwanaharamu apite kila mtu aendelee kufanya michongo yake.
"Halafu pia siyo Killy na Cheed tu, hakuna msanii aliyewahi kuwa hapo akarudisha pesa kwa sababu hapo hakujawahi kuwa na mifumo wala misingi ya urudishwaji pesa zaidi ya wewe mwenyewe tu ndio uliyekuwa ukiingiza pesa.
"Mlishawahi kunikatalia kufanya shoo ya sh milioni 10 na mpaka advansi sh milioni 5 ilishaingizwa kwenye account ya ofisi na huyo mtu nilimleta mpaka kwako masikini ya Mungu sikuwa hata na mia, mama yangu mzazi anaumwa nyumbani.
"Wadogo zangu wamerudishwa nyumbani ada hakuna nikasema na mimi nipate rizki ila show mliikataa nakumbuka hiyo siku nilivyorudi nyumbani nililia sana sababu mpaka leo sijawahi kujiua.
"Mungu alivyokuwa fundi sasa toka nimeanza kujitegemea mwenyewe nimeshaingiza zaidi ya sh milioni 40 na imetokana na muziki wangu huu huu.
"Nimenunua gari yangu kwa pesa yangu mwenyewe mpaka nimeanza na ujenzi wa nyumba kitu ambacho sikuwahi kukitegemea kabisa kulingana na hali ilivyokuwa huko," amesema Killy, Msanii wa muziki Tanzania.