Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), limeeleza sababu ya kumuita msanii Dulla Makabila kuwa imetokana na maudhui ya kutumia kiongozi wa dini katika wimbo wake wa ‘Pita Huku’
Wimbo huo Dulla ameuachia jana, ambapo ndani yake inaonyesha vitendo viovu ambavyo watu wamekuwa wakivifanya visivyompendeza Mungu na kuwaelekeza njia ambayo watapaswa kuingiwa kutokana na wanayoyafanya.
Akizungumza na Mwananchi Digital leo Jumatano Desemba 21,2 022, Katibu Mtendaji wa Basata, Dk Kedmon Mapana, amesema wimbo huo ni mzuri ila kasoro yake ipo katika maudhui ya kumtumia kiongozi wa dini.
“Hatuna shida na wimbo kwani ni mzuri na una ujumbe muri kwa jamii, shida ipo katika kiongozi wa dini alipotumiwa, kwani watu wako very sensitive (makini) na dini zao na baadhi wameshalamika kwa nini watumike wao.
“Hivyo tulichokifanya ni kumuita kijana wetu kumuelewesha wanapofanya haya, wajaribu kuwa makikini na imani za watu na wakati mwingine hata kutushirikisha tuwapeushauri kwanzakablahawajaichia nyimbo,” amesema Dk Mapana.
Hata hivyo alipoulizwa kama kuna mpango wa kuizuia hiyo nyimbo isionyeshwe kutokana na hilo, Katibu huyo alisema hawana mpango wa kuifungia isipokuwa walichokifanya ni katika kukumbushana na wasanii wajibu wao.