Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kili Paul aula tena India

Kili Paul Dsfc Kili Paul aula tena India

Wed, 5 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtengeneza wa Maudhui maarufu nchini Tanzania, ambaye amejizolea umaarufu mkubwa kwenye mtandao wa Tiktok pamoja na Instagram maudhui ambayo yalimfanya ajizolee mashabiki wengi huko India, @kili_paul mmasai huyu mkazi wa Chalinze unaweza kusema shavu limemdondokea.

Siku ya jana Kili Paul ametokea kwenye Tv shoo maarufu zaidi huko India inayofahamika kama 'Big Boss 16', uzito wa shoo hii ni kwamba inaongezwa na Mcheza filamu Mkongwe India Salman Khan.

Unachotakiwa kufahamu ni kwamba Kili Paul kwenye shoo hii alitokea kama Suprise kitu ambacho kiliibua Furaha kwa Mashabiki ambao walikuwa wakitazama show hiyo

Mmasai huyu anakula shavu hili mara baada ya siku 6 tu kushaare na mashabiki zake kupitia ukurasa wake wa instagram alisema kuwa yupo safarini anaelekea india.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live