Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kili Paul anapepea tu India, apata dili jingine tena!

Merge 1 Kl Kili Paul anapepea tu India, apata dili jingine tena!

Thu, 6 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya Big Boss na Meta Event, Mtanzania Kili Paul aalikwa tena kama mgeni maalum katika show nyingine kubwa India na kukutana na Madhuri Dixit superstar wa filamu za kihindi na kucheza pamoja.

Kili Paul amealikwa katika show maarufu ya vipaji vya kucheza Jhalak Dikhhla Jaa msimu wa 10 ambapo anaonekana akicheza na staa huyo mkubwa huku akimuelekeza namna ya kucheza wimbo toka katika filamu yake ya Anjaam(1994) aliyoigiza na Shah Rukh Khan.

Hi ni nafasi ambayo ameikosa Neema Paul kwani aliwahi kukaririwa akisema kwa waigizaji wa kike India humuambii kitu kwa Madhuri Dixit kwa jinsi anavyompenda.

Show hiyo inayotengenezwa na BBC Worldwide Productions Company, majaji wake wakuu ni 3 ambao ni Madhuri Dixit, Nora Fatehi aliyeshirikiana na Rayvanny katika wimbo wa Pepeta, jaji mwingine mkuu ni Karan Johar ambaye ni director na producer mkubwa katika filamu za Kihindi kupitia Dharma Productions ambapo pia ametengeneza na kuongoza filamu maarufu zikiwemo Kuch Kuch Hota Hai, Kal Ho Na Hoo, My Name Is Khan, Khabh Khush Khabhie Gham etc

Madhuri Dixt ambaye wiki hii ameripotiwa kununua nyumba mpya kwa kwa gharama ya crore 48 ambazo sio chini ya shilingi bilioni 13.6 za Tanzania, ametamba sana na filamu nyingi zikiwemo Koyla, Dil To Pagal Hai, Beta, Khalnayak, Devdas na series yake mpya ya Netflix hivi karibuni aliyoigiza kama mwigizaji mkuu ilikuwa yenye mafanikio.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live