Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kikwete awaza kutoboa Kimataifa

Jakay Mrisho Kikwete Rais Mstaafu wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete

Mon, 30 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Mstaafu wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alikuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya Uzinduzi wa Album ya marioo Ijumaa iliyopita katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar Es Salaam.

Kwenye hotuba yake fupi, Dkt. Kikwete alimpongeza Marioo kwa hatua kubwa ambayo amepiga kwenye Muziki wake lakini pia aliipongeza Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo pamoja na Baraza la Sanaa la Taifa.

Kwenye pongezi hapakosi ushauri, Dkt. Kikwete aliiomba Wizara kwa kushirikiana na BASATA kukuza sanaa kwani kwenye mataifa ya wenzetu kama Nigeria, sanaa inachangia pato la Taifa kwa asilimia kubwa sana. Aidha hakusita kuwaomba waivushe mipaka sanaa yetu kwani hapo ndio changamoto ilipo, Tutatoboaje Kimataifa?

“Kwa Nigeria, Sanaa inachangia pato la Taifa kwa asilimia kubwa sana, na sisi inawezekana. Changamoto yetu ni namna gani tutaufanya muziki wetu na filamu zetu zitoke zipate hadhi ya Kimataifa. Tutatoboaje huko katika anga za juu zaidi. Hiyo ndio iwe changamoto yetu, tukifanikiwa hilo mambo mazuri zaidi.” alisema Dkt. Kikwete na kuwata BASATA kuwaelekeza zaidi wasanii kuliko kuwaadhibu kila mara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live