Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Kikwete ahudhuria shughuli ya wajukuu zake kuhitimu jando Msoga

Jandooo 2802 Kikwete ahudhuria shughuli ya wajukuu zake kuhitimu jando Msoga

Thu, 4 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchana wa tarehe 31 Desemba 2023 kijijini Msoga wilaya ya Chalinze mkoani Pwani ukoo wa Kikwete walikuwa na sherehe kubwa  ya jando na unyago.

Sherehe hiyo ilihusisha  wavulana 11 na wasichana 7, wakiwemo watoto wa  Ridhiwani Kikwete, Mbunge wa Chalinze na Naibu Waziri katika Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, na ndugu zake.

Wavulana na wasichana hao waliotoka siku hiyo ni wajukuu wa Rais Mstaafu  Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na  kaka zake na dada zake.

Sherehe hizo zilizofana sana kwa nyimbo na ngoma za kitamaduni zilifanyika baada ya vijana hao kumaliza takriban wiki mbili za mafunzo maalum kwenye kambi yao porini kwa mujibu wa mila na desturi za kabila la Wakwere.

Kwa mujibu wa wanakijijij wa Msoga waliohudhuria sherehe hizo, Wakwere bado wanaendeza mila ya jando na unyago kwa wavulana na wasichana wao ili kulinda na kudumisha kwa vitendo mila na desturi zinazohakikisha mtoto au kijana wao, kabla ya kuingia katika umri wa ki-utu uzima, anapata maarifa au stadi za maisha zinazomfanya awe kijana shupavu, anayejitambua na anayewajibika kikamilifu katika jamii na taifa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live