Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiki za wasanii zamuibua Bashungwa

6ee031be8e6cdfcb0e0ef85babcc5c34.jpeg Kiki za wasanii zamuibua Bashungwa

Sun, 18 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

SERIKALI imesema kuwa itachukua hatua kali zaidi dhidi ya wasanii wanaotumia mitandao ya kijamii kudhalilishana.

Hayo yalisemwa juzi na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa (pichani) wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kiki wanazofanya wasanii katika mitandao.

Alisema Serikali itahakikisha wasanii kupitia sanaa yao wananufaika nayo pamoja na wale waliowaajiri.

Alisema anatoa wito kwa wasanii kuendelea kuzingatia maadili na ajafurahishwa na yale yanayoendelea katika mitandao ya kijamii, kwani ni ya kitoto na yako kinyume na maadili.

Alisema yale yanayoendelea mintandaoni kwa sanii ni ya kitoto na serilali

imewataka kuacha mara moka tabia hyo ili iweze kuwaendeleza wasanii kupitia sanaa zao na wakiendelea na utoto wao huo, adhabu kali zitatolewa kwa wale watakaoendelea kufanya hivyo.

Alisema amechukizwa sana na kile ambacho kinafanywa na wasanii, hivyo ameliagiza Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kulishughuliia hilo na tayari ametoa onyo kwa wasanii wenye tabia hiyo.

Amewataka wasanii kujenga tabia ya umoja na mshikamano na hayo yanayoendelea mitandaoni ni ya kitoto na ni jambo la kuchafuana tu.

Aliwataka wasanii kundokana na mambo hiyoambayo aliziita kuwa ni za kitoto na kusisitiza kuwa adhabu kali itatolewa na hataki kuona watu wanajitokeza kufanya ujinga huo.

Alisema kuwa hatakiona wasanii wakifungiwa wana-

jitokeza watu kuwaombea msamaha wakitaka kuondolewa adhabu.

“Tunataka wasanii wote nchini wanufaike na sanaa yao, haya yanayoendelea mitandaoni ni ya kitoto waondokane nayo, kwasababu serikali tumedhamilia kuhakikisha wasanii na wale ambao wako tayari wanufaike na sanaa yao…”

Alitoa wito kwa wasanii kuendelea kuzingatia maadili na tamaduni za kiafrika, huku akisisitiza kuchefuliwa na yake yanayoendelea katika mitandao ya kijamii.

Wakati huohuo, Waziri Bashungwa amesema kuwa wizara yake katika bajeti inayokuja mwaka huu, wamepanga kutenga kiasi cha Sh bilioni 1.5 kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Sanaa na Utamaduni, na ana matumaini itapita, kwani hakuna mbunge asiye na msanii jimboni kwake.

Chanzo: www.habarileo.co.tz