Kijiji cha Salto de Castro kilichopo nchini Uhispania kinauzwa kwa pauni 259,000.
Kijiji hiki kilichopo katika eneo hili la jimbo la Zamora lililopo kwenye mpaka na nchi ya Ureno, kina majumba maarufu ya watu wa Uhispania.
Miongoni mwa nyumba za kijiji zipatazo 44, kuna hoteli, nyumba za kuishi, kanisa, shule na dimbwi la kuogelea pamoja na kambi ya kijeshi.
Hatahivyo, tatizo la kijiji hiki ni kwamba hakuna mtu anayeishi huko na kimetelekezwa kwani watu walikihama zaidi ya miaka 30 iliyopita.
Mmiliki wa kijiji hicho alikinunua mwanzoni mwa karne hii na alitaka kukifanya kiwe eneo la utalii, lakini mzozo wa eneo la ulaya ulizuia mpango huo.
Watu wengi wameelezea haja ya kukinunua kutokana na bei yake ya chee.
Ronnie RodrÃguez, ambaye ni mwakilishi wa mmiliki wa kijiji hiki, amesema kuwa watu 300 wameelezea nia ya kununua kijiji hicho. Watu hao wanatoka mataifa ya Urusi, Ufaransa, Ubelgiji na Uingereza.
Baadhi hata wamelipa malipo ya awali ili kisichukuliwe na wanunuzi wengine, kulingana na RodrÃguez.