Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kijana ajinyonga kisa 'Dear Ex' ya Marioo

Mauaji?fit=600%2C400&ssl=1 Kijana ajinyonga kisa 'Dear Ex' ya Marioo

Wed, 25 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kijana Jumaa Khamisi (32) amefariki dunia mara baada ya kujinyonga katika kijiji cha Kipumbwi Mji Mkuu Wilayani Pangani Mkoani Tanga huku ikihisiwa kuwa chanzo ni stress za kimapenzi kwakuwa Jumaa aliachana na Mpenzi wake na saa kadhaa kabla ya kujinyonga alisikiliza wimbo wa Dear X ya Marioo kwa takribani mara 60 na alipoambiwa inatosha akachukia na kuondoka.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kipumbwi Mji Mkuu, Mwanaidi Abbasi amesema kabla ya tukio hilo Jumaa alifika nyumbani kwake majira ya saa moja asubuhi kufata vitafunio ndipo baadaye jioni alipopata taarifa za tukio hilo la kujinyonga kwa kijana huyo

“Wakati namwandalia vitafunio aliingia ndani kwangu akawa anaangalia TV na nyimbo ambayo alichagua ni Dear X, alisikiliza kariba mara 60 ile ambayo Msanii anaimba nikimrudia EX wangu bora kufa”

Kwa upande wake Haji Said ambaye ni Rafiki wa marehemu amesema mara ya mwisho kuachana na Jumaa alimuaga anaenda kupumzika lakini hakumueleza changamoto yeyote ambayo inamkabili

“Sisi tunadhani chanzo ni mapenzi maana alikuwa na Mtu wake kwakweli wakapanga mipango yao hadi wanamaliza aliingia kidudu mtu kati ndio akakavuruga fulani hivi nadhani hicho ndo chanzo kikubwa.’’

Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga kupitia kwa Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Maketi Msangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema limetokea Oktoba 22, 2023 ambapo Jumaa alijinyonga na chandarua kwenye chumba cha mdogo wake hadi kupelekea kufariki.

Hata hivyo Kaimu Kamanda wa Polisi amesema Jumaa alikuwa Mtumiajii mkubwa wa dawa za kulevya kama vile heroin na pombe kali na hivyo Polisi inaendelea na uchunguzi kuweza kufahamu chanzo cha tukio hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live