Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiingilio kuwaona Sauti Sol ni Tsh. 344000

Bien Solccc Kiingilio kuwaona Sauti Sol Tsh 344000

Tue, 29 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii kiongozi wa bendi ya Sauti Sol, Bien amefichua sababu ya kuweka kiingilio cha KSh 20,000 (Takribani TSh. 344,000) kwenye shoo yao ya mwisho kabisa pamoja kama kundi.

Katika mahojiano na Mungai Eve, Bien alisema kwamba licha mashabiki wao kulia kwamba kiingilio hicho ni cha hali ya juu sana na uchumi umezorota, lakini pia wao wana sababu ya kutoza kiingilio hicho akisema kuwa pia uchumi umekula upande wao vile vile.

“Ni kweli uchumi ni mbaya hata kwetu kusema kweli, kwa sababu gharama ya kila kitu katika tamasha hilo pia imepanda juu. Unajua mafuta yakipanda bei yanaathiri kila kitu mpaka chini. Kuna vigezo vingi sana ambavyo vinasababisha sisi kuweka bei ya tikito hiyo.” alisema Bien.

Bien hata hivyo aliwataka Radhi mashabiki akiwaomba kuwa waelewa kuwa hata wao si kwamba wanataka kuwalaghai wala kuwatapeli.

“Tungeomba mashabiki tafadhali mtuelewe. Poleni sana. Hatujaribu kuwachukulia poa lakini pia tunawapatia miaka 20 ya maisha yetu ya kimuziki pamoja, mkituona kweye jukwaa, hiyo tiketi ni ya thamani ya miaka 20 yetu kuwa pamoja.” alisema Bien.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live