Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Kigwangalla akubali yaishe kwa MO

8f12fbb03dae896f081a7233583580ed Kigwangalla akubali yaishe kwa MO

Sun, 22 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MBUNGE wa Nzega mkoani Tabora ambaye ni mwanachama wa Simba, Dk. Hamisi Kigwangalla amemuomba radhi mwekezaji wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji ‘MO’ kutokana na sintofahamu iliyotokea hivi karibuni.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Dk Kigwangalla aliandika amekuwa akiwaza juu ya kusameheana na Dewji ili wasonge mbele, hivyo ametumia nafasi hiyo kuwaomba radhi mashabiki wa Simba pamoja na MO ili maisha yaendelee.

"Wanasimba tunataka ushindi dakika 90 uwanjani na mchango wa MO siyo wa kudharau, lakini hata yeye na biashara zake wanafaidika na Simba kama ‘brand', siyo bure. Thamani ya Simba siyo majengo, ni ‘brand’ yenye umri wa zaidi ya miaka 80", aliandika Dk Kigwangalla.

"Nimekuwa nikiwaza juu ya kusameheana, yaishe tusonge mbele. Naomba radhi kwake na kwa washabiki wote wa Simba niliowakwaza. Mimi nimesamehe. Maisha yaendelee", ameongeza.

Wawili hao waliingia katika malumbano ya maneno mitandaoni kuhusu suala la uwekezaji ndani ya Simba, baada ya Dk. Kigwangalla kuhoji masuala kadhaa ikwemo Bilioni 20 ambazo MO anatakiwa kuziweka kwenye akaunti ya klabu kama kiasi cha uwekezaji ndani ya klabu kwa mujibu wa makubaliano.

Baada ya kuhoji, MO aliibuka na kumjibu Dk Kigwangalla akihusisha na mkopo wa pikipiki ambao Dk. Kigwangalla aliomba kwake, ndipo muendelezo wa kauli mbalimbali ulipoanzia.

Mchakato wa uwekezaji ndani ya Simba bado haujakamilika, ambapo hivi sasa Tume ya Ushindani nchini FCC imetoa maelekezo kwa klabu ya Simba kufuata taratibu zinazohitajika ili mchakato uendelee.

Chanzo: habarileo.co.tz