Mwigizaji maarufu kutoka Nigeria, Yvonne Jegede amesema kuwa itakuwa pigo kubwa kwa mfumo mzima wa mahakama ikiwa haki haitapatikana kuhusu kesi ya kifo cha Msanii Ilerioluwa Oladimeji Aloba maarufu kama MohBad.
Jegede Kupitia akaunti yake ya Instagram amesema; "Kesi hii ni kubwa sana kiasi kwamba ikiwa haki haitapatikana, itakuwa pigo kubwa Afrika na mfumo wake mzima wa mahakama. Ninawaamini Jeshi la Polisi Nigeria, najua wana utaalamu wa kushughulikia hili ikiwa wataamua na kutaka
"Mimi ninachokiomba ni afya ya akili ya kila mmoja wetu, tusaidie kutatua kesi hii kwa sababu dunia nzima inaifahamu kesi hii hasa. Na kuna mianya ya (ushahidi) mingi mtandaoni ya kutafuta watu wa kuchunguza maana haina ugumu huo."
Mohbad alifariki sep 12 Mwaka huu baada ya Kutoka Kwenye Show huko Ikorodu Nchini Nigeria.
Je, unaamini haki ya Mohbad itapatikana kwa hiki kinachoendelea mitandaoni?