Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kifo cha Gamba kimegusa wengi

Wed, 31 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkuu wa idara ya kiswahili ya shirika la utangazaji la Ujerumani DW Deutsche Welle Andrea  Schmidt amesema kifo cha Gamba  kimegusa watu wengi ndani na nje ya Afrika.

Akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya Shirika la utangazaji la Ujerumani leo Oktoba 29 Schmidt amesema taarifa hizo ziligusa watu wengi ikiwamo Marekani.

"Kifo cha Isaac kimegusa watu wengi baada ya kupata taarifa zilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kwa kasi sana nakuanza kupokea pole  nmkutoka Mataifa mbalimbali," amesema Schmidt.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akitoa salamu za rambirambi amewataka waandishi wa habari kudumisha umoja na kujikita katika uchumi imara.

"Marehemu Gamba ni miongoni mwa waandishi walionipa umaarufu nje ya nchi niwashauri kudumisha umoja na kujikita katika uchumi imara," amesema Makonda.

Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe amesema amesema marehemu alikuwa ni mtu mwene msimamo akisimamia jambo lake lazima liwe.

"Marehemu Gamba alikuwa ni mcheshi, mnyenyekevu lakini alikuwa ni mtu mwenye msimamo alikuwa akiamua kusimamia jambo lake lazima liwe," amesema Gondwe.

Akisoma wasifu wa marehemu, mtangazaji wa Redio One Regina Mwalekwa amesema Gamba alizaliwa january 19, 1970 wilayani Bunda-mjini alipata elimu yake ya msingi, katika shule ya msingi Kabalimu iliyoko mjini Bunda kuanzia mwaka 1978 nakuhitimu mwaka 1984.

Baadaye aliendelea na masomo ya Sekondari katika shule ya sekondari Majengo Moshi kuanzia mwaka 1985 hadi mwaka 1988 na baadaye kuendelea na masomo ya A Level katika shule ya Old Moshi kuanzia mwaka 1989 hadi mwaka 1991.

 

Marehemu alianza kufanya kazi kwa muda wa takribani miezi sita akiwa Arusha katika Radio 5, na ndipo kwenda kujiunga na kituo cha utangazaji cha Radio Free Africa (RFA) Mwanza mwaka 1997s mpaka mwaka 2003, kisha akajiunga na Redio Uhuru ya jijini Dar es Salaam mwaka 2004.

 

Amesema mwaka 2005 alijiunga na kampuni ya IPP na  alifanya kazi  hadi mwaka 2015 alipohamia katika shirika la utangazaji Ujerumani la Deutsche Welle (DW).

 

Baada ya uchunguzi iligundulika kuwa kilicho sababisha kifo chake ni kuvuja kwa damu kwenye ubongo yaani Presha ya Damu.

 

Oktoba 18,2018 Gamba alikutwa akiwa amefariki chumbani kwake baada yakutoonekana kazini kwa siku mbili.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz