Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kifo cha AKA, baba mkwe atoa ya moyoni

Mosws Tembe.jpeg Kifo cha AKA, baba mkwe atoa ya moyoni

Sun, 12 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

FAHAMU Kifo cha Rapa Kiernan Forbes maarufu kama AKA kutokea Afrika Kusini siku ya jana, kimerudisha tena story ya kifo cha mpenzi wake za zamani Anele “Nelli” Tembe ambaye alifariki April 2021 kwa kujirusha kutoka ghorofani.

Baba mzazi wa Nelli, Mfanyabiashara Moses Tembe ambaye makazi yake yapo katika mji wa Durban aliposhambuliwa AKA kwa risasi, ameongea na chombo cha habari cha TimesLive na kusikitishwa na taarifa ya kifo cha AKA na kutoa pole kwa familia ya AKA.

"Kiernan alikuwa mwanamuziki mwenye kipaji cha ajabu, muziki wake ulileta mchango mkubwa mkubwa Afrika Kusini, tunatoa pole kwa familia yake na mashabiki wake," amesema Moses Tembe.

Baadhi ya mashabiki mitandaoni nchini humo walianza kumuhusisha Moses Tembe kwenye kifo cha AKA. Binti yake Nelli kabla ya kifo chake alikuwa kwenye mahusiano na AKA na walikuwa pamoja hotelini siku aliyojiua.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live