Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kidumbaki, taarabu asilia kukonga nyoyo tamasha la chakula la Stone Food Festival Zanzibar

Wed, 2 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.  Taarabu  asilia  na ngoma ya kidumbaki zimetajwa kuwa miongoni mwa burudani zitakazonogesha na kupamba tamasha la Stone Food Festival Zanzibar litakaloanza  Oktoba 11 hadi 19, 2019 visiwani humo.

Tarehe hiyo inakwenda sambamba na kalenda ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (Unesco), linalosherehekea tamasha la siku ya vyakula duniani kila mwaka.

Kwa upande wa Zanzibar,  tamasha hilo ni la nne tangu kuanzishwa kwake na limepewa jina la Stone Food Festival Zanzibar, likiandaliwa na wamiliki wa hoteli, migahawa, zaidi ya 30.

Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam leo Jumanne Oktoba 1, 2019 mmoja wa waandaaji tamasha hilo, Shabnam Salim wa mgahawa wa  Café Tourquoise, uliopo Stone Town amesema tamasha hilo ni muhimu na linahamasisha ulaji wa vyakula.

“Watalii na wenyewe wataburudika na muziki huo wa asili Visiwani humo, lakini wakifurahia vyakula mbalimbali maarufu na  pia watapara fursa ya kuvitayarisha,” amesema.

Salim amesema tamasha hilo siku tatu za mwanzo litafanyika katika viwanja vya Forodhani kuanzia saa 12 jioni ambapo waandaaji wataonyesha na kuuza vyakula mbalimbali vya asili viliyoandaliwa kwa ubunifu.

Pia Soma

Advertisement
Amesema baada ya siku tatu kukamilika tamasha hilo litaendelea kwa wenye hoteli au migahawa kuliendeleza katika maeneo ya kazi hadi siku ya kilele chake Oktoba 19, 2019.

Chanzo: mwananchi.co.tz