Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Kiboko aliedhaniwa Dume kwa miaka 7 agundulika kuwa jike

Kiboko Dume X Jike Kiboko aliedhaniwa Dumbe kwa miaka 7 agundulika kuwa jike

Wed, 24 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hifadhi moja ya wanyama nchini Japan imethibitisha kuwa kiboko mmoja aliyedhaniwa kuwa ni dume kwa miaka saba, kuwa ni jike.

Uchunguzi wa vinasaba – DNA- ulifanywa na hifadhi hiyo baada ya wafanyakazi kuona kuwa mnyama huyo aitwaye Gen-chan kutoonesha tabia zozote za kiboko wa kiume.

Gen-Chan aliwasili mjini Osaka mwaka 2017 akitokea Mexico, na nyaraka za forodha wakati huo zilionesha kuwa alikuwa kiboko wa kiume.

“Tutaendelea kufanya kila tuwezalo kumpa mazingira mazuri Gen-chan,” imesema hifadhi hiyo.

Hifadhi, au bustani ya wanyama ya Osaka Tennoji ilithibitisha taarifa hizi kupitia tovuti yake wiki iliyopita.

Taarifa hiyo ilisema Gen-chan aliwasili Japan akitokea Mexico wakati akiwa na umri wa miaka mitano na akitajwa jinsia yake kuwa ya kiume.

Taarifa hiyo imesema kwa sababu Gen-chan alikuwa bado mdogo wafanyakazi wa hifadhi hawakutilia shaka nyaraka hizo.

Lakini wafanyakazi hao walianza kupata wasiwasi baada ya Gen-chan kuwa mkubwa kwa sababu hawakuweza kuona viungo vyake vya uzazi.

Msemaji wa hifadhi hiyo ameliambia shirika la habari la AFP siku ya Jumanne kuwa tabia ambazo Gen-chan hakuwa akionesha ni pamoja na kutoa milio ya kuita viboko wa kike na kutawanya kinyesi chake kama ishara ya kuweka alama ya himaya yake.

Hifadhi hiyo imesema jina la Gen-chan halitabadilishwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live