Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kibibi: Watu wananiogopa

Kibibi (1).png Kibibi: Watu wananiogopa

Mon, 21 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwigizaji Getrude Mwita aliyejipatia umaarufu kwa kuigiza uhusika wa Kibibi katika Tamthilia ya Huba, amekuwa akipata wakati mgumu kuishi na jamii yake kwani wengi wao wanahisi ni mwanamke katili kama anavyoigiza kwenye tamthilia hiyo.

Akizungumzia hilo, Kibibi amedai kuwa kuna wakati hata akikutana na watu mtaani au maeneo yoyote wanamkimbia wakidhani kuwa atawadhuru kutokana na uhusika wake ambao amekuwa akiuonyesha kupitia tamthilia hiyo maarufu.

"Kutokana na uhusika wangu ninaoigiza kwenye tamthilia ya Huba, imekuwa ngumu kupata mpenzi kwasababu wanaume wananiogopa, wanahisi kama mimi ni katili kupitiliza, ile ni kazi tu jamani, mimi siko hivyo.

"Kwa hiyo sasa hivi niko single na muda wangu mwingi nautumia kufanya mazoezi ili kujiepusha na stress baada ya kuachwa hivi karibuni," amesema Kibibi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: