Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiben'teni: Kwa Zari najihisi mwenye bahati

Zari 7 Kiben'teni: Kwa Zari najihisi mwenye bahati

Wed, 28 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zari The Boss Lady; ni mwanamitindo na mfanyabiashara maarufu Afrika Mashariki ambaye Ijumaa iliyopita alikuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa na watu mbalimbali walijumuuika naye kumtumia jumbe za heri njema.

Mmoja wa watu waliomtakia heri njema ni mpenzi wake mdogo kiumri (kiben’teni) aitwaye Shakib Cham.

Kijana huyo ambaye hivi majuzi Zari alidokeza huenda ndiye mwanaume wake wa mwisho kuchumbiana na yuko tayari kumtolea mahari, amemsifia Zari kwa ujumbe maridhawa akimtaja kama malkia katika himaya ya moyo wake.

“Furaha ya siku ya kuzaliwa malkia wangu, siku hii iwe ya kweli na ya kushangaza kwako mrembo wangu! Nakupenda siku zote na daima na milele!! Najihisi kuwa na bahati kuwa na wewe mtoto,” anasema Shakib Cham akisindikiza na picha zao za pamoja.

Zari ambaye ni baby mama wa msanii Diamond Platnumz, hakutulia kwani alifika kwenye picha hizo na kumjibu kimahaba huku akisema kamwe hawezi kumuacha na kuwa anajihisi furaha na amani ya nafsi kuwa na yeye.

“Asante mpenzi wangu. Nakupenda sana babe…” Amejibu Zari ambaye ni mama wa watoto watano.

Hivi karibuni Zari alijikuta kwenye majibizano makali na watu mitandaoni waliokuwa wakimsuta kwa kuanza mahusiano na kijana mdogo ambaye amemuacha kiumri maradufu.

Zari alijitetea kwamba hata wanaume huwa na hulka ya kuingia kwenye mapenzi na wasichana wadogo kuwaliko kiumri na halijawahi kuwa tatizo, lakini ikija kwa upande wa wanawake kuwa kimapenzi na vijana wadogo, basi ni gumzo zito.

Zari alitangaza kuwa kijana wake, Cham wako tayari kuongozana kuona wazazi wake na ikiwezekana kumtolea mahari kama mkewe wa kupika na kupakua.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live