Taarifa mpya kutoka kwenye tasnia ya muziki wa Bongo ni kwamba, lebo ya muziki nchini Kings Music Records inayomilikiwa na staa wa Bongo Fleva, Alikiba imemtambulisha msanii wake mpya anayefahamika kwa jina la Vanillah Music.
Msanii huyo chipukizi ni miongoni mwa wasanii wachanga ambao wanakubalika sana na Alikiba ambapo ameshriki kwa sehemu kubwa kuandika ngoma UTU ya Alikiba na baadhi ya ngoma kwenye albam ya Kiba.
Utambulisho huo wa Vanillah unakuja ikiwa ni takribani mwezi mmoja tangu waliokuwa wasanii wa King Music kisha kwenda Konde Music, Killy na Cheed kuachana na Konde Gang huku mashabiki wakiwasihi warudi Kings Music.