Wazungu wanasema 'Form is temporary but Classic is Permanent' ndicho alikionesha King Kiba @officialalikiba kuonesha tofauti kati ya msanii na mwanamuziki kwenye stage ya @lockin255 pale The Super Dome Masaki.
Ilikua show Classic sana ya muziki mzuri kutoka kwa Kiba aliyeimbisha mashabiki kwa saa 2 na dakika zake stejini na kuperforme Hits zake zote.
Hakutumia nguvu ya mashabiki kuwaambia kuweka mikono juu, twende kulia, kushoto au kupiga kelele ili kupata vibes na energy aliacha kazi ya muziki wake na performance yake iongee kwenye stage bila kuboreka.
Ubunifu wa kufanya 'Mash Up' ya ngoma zake kwenye bendi utaona kama Mahaba imepigwa kwa style ya muziki wa rege, sebene la Mwana na Dushelele, kutetema kama Mayele na kupigishwa Amapiano.
Pia Kiba amefanya jambo la kukuza muziki wa BongoFleva kwenye shows za kimataifa kama ile aliyofanya mbele ya @ayrastarr kwa kupandisha wasanii kama @marioo_tz @tommyflavour @vanillahmusic @jaivah @chinokidd7 na @mimi_mvrs11 ambao huenda ikawa Platform kwao kwa walichokifanya.
DC Nikk wa Pili, Hamisa Mobetto, Kajala, Paulah, Marioo, Abbah, Jaivah ni baadhi tu ya mastaa waliojitokeza kujionea show hii ya Alikiba na Ayra Starr kwenye stage moja.