Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiba, Rayvanny wamzuia Jay Melody kuachia ngoma

KIBA DIAMOND Jay Melody ajibu kuhusu Kiba, Rayvanny kukwamisha ngoma yake

Thu, 21 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii chipukizi wa muziki wa Bongo Fleva, Jay Melody amesema hatoachia hewani kamwe remix ya ngoma yake ya Huba Hulu, ambayoo moja amefanya na Rayvanny na nyingine Alikiba wanatajwa.

Jay amedai anawapenda sana wasanii hao wawili na kila mmoja amemshawishi kwenye muziki wake lakini imefika hatua yeye ndiye atabaki kuwa mtu mwenye maamuzi ya mwisho kwenye hilo.

"Hakuna remix yoyote ambayo ya Huba Hulu kati ya ile niliyofanya na Rayvanny ama niliyofanya na Alikiba, lazima watu niwaambie ukweli. Msanii ukiwa unatoka unakutana na changamoto nyingi sana, kwa kipindi kile uwezekano wa kufanya remix ulikuwa mkubwa lakini haya mambo timu flani na timu flani yanaharibu sana," amesema Jay Melody.

Jay amedai kuwa muziki wa Bongo umejaa matabaka yaliyo tengenezwa na wasanii wakubwa kwenye tasnia, na utaendelea kuwaumiza wasanii waliopo kwenye game na hata wanao kuja kwa sababu inatengeneza uadui kwa msanii mmoja kufanya kolabo na msanii mwingine.

"Rayvanny alivyopost ile picha tupo studio tunarekodi ilileta tension kubwa sana, nilikuwa kwenye stress kubwa mpaka nikazima simu siku nzima, kwa hiyo sitoachia remix yoyote sitaki kuwagombanisha watu. Kuna remix nimefanya na Marioo ni msanii mkubwa, watu waendelee ku-enjoy," amesema Jay Melody.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live