Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiba, Mwasiti hawanipigii simu - Chid Benz

Chid Benz Kms Chid Benz.

Wed, 13 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Hip Hop Chid Benz amesema kuwa wapo baadhi ya wasanii ambao licha ya yeye kujitoa kuwasaida lakini wamekuwa hawamjali wakati akiwa katika changamoto za maisha.

Chid amesema watu wengi akiwataja wasanii wenzake Alikiba na Mwasiti hawana huruma na maisha yake wanaigiza tu huko mitandaoni kuwa wanania ya kumsadia lakini hamna wanachokifanya kumsaidia.

“Ngoja nikwambie mdogo, Mwasiti nilimkuta Studio za 41 Record kwa Lamar wakati naenda kurekodi wimbo wangu na K-Lynn. Mwasiti akasema ilikuwa arekodi wimbo wake na Profesa jay kama mbadala wangu baada ya kuambiwa na Bosi Ruge kwamba kumpata Chid ni ngumu, mimi nilirekodi naye lakini mbona hanipigii simu?

"Alikiba nimefanya naye ngoma kama mbili au tatu, akaachia albamu yake, mbona hanipigii kwamba broo hivi na hivi nakusaidia hivi? Hawa watu hawana huruma na mimi,“ alisema Chid Benz.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live