Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Khaligraph Jones, Nyashinski kuamsha popo na Rick Ross Kenya

7117 Z Bongo5 Rick Ross TZW

Thu, 26 Apr 2018 Chanzo: bongo5.com

Weekend hii inayokuja rapper kutoka nchini Marekani, Rick Ross anatarajiwa kufanya show ya kipekee nchini Kenya.



Show hiyo ambayo imeandaliwa na NRG Radio itafanyika April 28, 2018. Rick Ross anatarajiwa kupanda jukwaani na Khaligraph Jones na Nyashinski kutoka Kenya.

Hii itakuwa ni mara ya pili kwa Rick Ross kufanya show Afrika Mashariki, kwa mara ya kwanza alifanya show Tanzania mwaka 2012 katika tamasha la Fiesta.

Rick Ross anagonga vichwa vya habari tena Afrika Mashariki ikiwa ni miezi minne imepita tangu ashirikishwe na Diamond katika ngoma yake inayokwenda kwa jina la Waka.

Chanzo: bongo5.com