Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Khadija Kopa avifumbia macho vibeniten, kisa?

5188 26864041 1615943441854897 5164600746401857536 N TZW

Thu, 22 Mar 2018 Chanzo: bongo5.com

Msanii wa muziki wa taarab nchini, Khadija Kopa amesema moja ya vitu ambavyo havipendi ni kuwa katika mahusiano na mtu mdogo kwake kiumri.



Muimbaji huyo ameiambia Kikaangoni, EATVkuwa licha kutopenda jambo hilo lakini isiwe sababu ya kuwasema vibaya wanawake waliyo katika aina hiyo ya mahusiano.

“Mbona nyinyi wanaume wazee mnaoa wanawake wadogo na sisi hatusemi, sisi kila siku vibenteni vibenteni. Babu wee, mimi sipendi viben ten, mimi nilikuwa na mume wangu, na hata ikiwa dini yetu inaruhusu Mtume wetu alituonyesha njia,” Khadija Kopa.

Katika hatua nyingine Khadija Kopa ameongeza kuwa baada ya mume wake kufariki kipindi kirefu, yeye yupo tayari kuolewa ila na mtu mwenye umri wa kuanzia miaka 40 ila asizidi sana.

Chanzo: bongo5.com