Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Khadija Kopa asisitiza kutojua mahusiano ya Zuchu na Diamond

 Khadija Kopa Asisitiza Kutojua Mahusiano Ya Zuchu Na Diamond.png Khadija Kopa asisitiza kutojua mahusiano ya Zuchu na Diamond

Wed, 22 Nov 2023 Chanzo: Radio Jambo

Khadija Kopa mwimbaji wa muziki wa Taarab na mtunzi wa nyimbo kutoka nchini Tanzania ambaye pia ni mamake mzazi msanii maarufu wa Bongo Zuchu kwa mara ya pili amezungumzia kutoyafahamu mahusiano ya ndoa kati Bintiye Zuchu na Nyota wa Bongo Diamond Platnumz

Kulingana na Khadija Kopa Bintiye Zuchu hajawai kumfahamisha wala kumtambulisha kwa Diamond akisimulia kuwa mapenzi yao wanayajua wao wenyewe.

"Siyajui kamwe mahusiano ya Binti yangu Zuchu na msanii Diamond nadhani ni siri yao na Muumba wao kwani sijawahi fahamishwa, kwa vyovote vile ikiwa ni mahusiano ya kweli waje nyumbani wajitabulishe kulingana na mila zetu,"alisema Khadija Kopa.

Mtunzi huyo wa Taarab alikiri hayo Kwenye mahojiano ya moja kwa moja na wanablogu wa mitandao akisema kuwa yeye ni mzazi ambaye upendezwa na utaratibu wa kufanya mambo hadharani, huku akitaja ikiwa Mwanawe yuko kwa Mahusiano ni lazima afuate mila na desturi kwani hawezi kamwe kukumbali ndoa ambayo hajafahamishwa.

"Siwezi kushawishiwa na kwa vyovyote mimi nina heshima Zangu kulingana na mila zetu mshichana anapopata mume lazima wazazi wajulishe kwa pande mbili zote ndiposa swala la kulipiwa mahari itekelezwe kwa wakati unaofaa kwa hivo Diamond na binti yangu Zuchu hawajaona," alisema Kadhija Kopa.

Hiyo ni mara ya pili kwa Khadija Kopa kukiri kuwa hayajui mahusiano kati ya bintiye Zuchu na msanii Diamond.

Chanzo: Radio Jambo