Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Khadija Kopa asingiziwa kuua mtu, ataja uchawi

Khadija Kopa Khadija Kopa asingiziwa kuua mtu, ataja uchawi

Wed, 22 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Staa wa muziki wa Taarab nchini Tanzania Khadija Kopa almaarufu Malkia wa mipasho ambaye pia ni mtunzi wa nyimbo amefunguka na kusema kuwa jambo ambalo lilimkera sana kwa maisha yake zaidi ni kusingiziwa kuwa aliua mtu.

Kwenye mahojiano ya moja kwa moja na mwanablogu wa mtandao mwimbaji huyo alisema kuwa jambo la wanamuziki kusemwa ni la kawaida ila kuna wakati hufika ikawa ni uchungu huku akirejelea  kwake ilikuwa uchungu kusingiziwa kuua mtu kwa kumroga.

"Nilikekwa mno baada ya kusingiziwa kuwa nilimuua mtu kwa kumroga jambo ambalo ilinikera sana kwa maisha yangu kwani ilikuwa tu taarifa ya huongo ili kuniarimbia jina langu kwenye taaluma ya muziki,"alisema Khadija Kopa.

Kulingana na nyota huyo wa muziki umekuwa ni mtindo  na jambo la kawida kwa wanamuziki maarufu kusemwa.

"Wanamuziki imefikia wakati ikabidi tukubali semi mbaya na kauli za uongo kwenye mitandao kwani umekuwa mtindo mpaka kwa sasa msanii asipotajwa sana jina lake halitang'aa sana ila kuna kauli zingine zinatokea kuaribia wasanii jina ambazo zinakera sana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live