Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Khadija Kopa afungukia bifu la Zuchu na Nandy

KOPA NA NANDY Khadija Kopa afungukia bifu la Zuchu na Nandy

Thu, 8 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Malkia wa Mipasho Bongo, Khadija Kopa amefungukia ishu ya mwanaye Zuchu kudaiwa kuwa kwenye toafuti na msanii mwenzake Nandy.

Kopa amesema alisikia ishu hiyo baada ya kuvuja kwa sauti za Nandy zikimhusisha Zuchu lakini alichukulia kwamba ni suala la kawaida tu katika muziki hivyo kumsihi hata mwanaye achukulie kawaida.

“Mimi kama mama najua huu muziki una mambo mengi hivyo nilimwambia atulie tu asijali,” alisema Khadija Kopa.

Iliwahi kuvuja sauti iliyosemekana ni ya Nandy akisikika akimueleza Mwijaku kuwa amepata dili la kinywaji fulani si kwa sababu Zuchu alilikataa kwa sababu ya kilevi kama alivyodai bali yeye alipambana mwenye kulipata na jina lake lilimbeba hivyo kuleta fununu kwamba wawili hao hawaivi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live