Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Khadija Kopa: Zuchu alipenda sanaa

F3f9e541f5e789f72766775893cf84e8 Khadija Kopa: Zuchu alipenda sanaa

Sun, 19 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MAMA mzazi wa msanii wa Bongo Fleva Zuhuru Kopa Zuchu’ ambaye ni msanii wa muziki wa taarabu Khadija Kopa amefi chua kuwa mtoto wake alikuwa anapenda sanaa tangu akiwa mdogo kipindi cha malezi yake.

Khadija Kopa alisema wakati malezi ya mtoto wake huyo, alipenda sana michezo na shughuli za sanaa na kwamba aliwahi kupata tuzo kadhaa kutokana na ushiriki wake mzuri kwenye kazi za sanaa.

“Alikuwa anapenda michezo, kuimba kucheza hata akiwa shule alipata zawadi nyingi kwa ajili ya sanaa na michezo,”alisema Khadija Kopa.

Alisema Zuchu hana tabia za ajabu kwani alimlea kwenye mazingira mazuri, na alikuwa anapenda kusoma na kuongeza kuwa shule yao ilipata tuzo maalumu kwa ajili ya mtoto wake.

Zuchu ni miongoni mwa wasanii wakike wanaofanya vizuri kwenye muziki wa Bongo Fleva, kwa kipindi kifupi alichokuwa kwenye sanaa, Zuchu alifanikiwa kuachia ‘Extended Play’ yenye nyimbo sita.

Chanzo: habarileo.co.tz