Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kevin de Bruyne alivyoporwa mpenzi na Thibaut Courtois

KDB THIBA Kevin de Bruyne alivyoporwa mpenzi na Thibaut Courtois

Wed, 13 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Picha ni marafiki wawili waliokua pamoja ndani timu ya kukuza vipaji nyumbani kwao Belgium mmoja wa kishua Thibaut mwingine wa maisha ya chini kabisa Kevin De Bruyne baadae wakanunuliwa na Chelsea ya vijana baadae mwanamke akawafanya kutengena na kuwa maadui mpaka leo na hawajawahi kusemeshana licha ya kua wanaitwa timu ya taifa.

Mwadada unaemwona pichani hapo amevalia uzi wa Real Madrid ni Caroline Lijnen, hapo awali alikua mpenzi wa Kevin De Bruyne na mwamba unaambiwa alimpenda sana na walipanga mambo mengi lakini kutokana na ujanja aliokua nao rafiki ake na KDB, Thibaut Courtois alimzunguka rafiki yake kipenzi kwa kumshawishi shemeji yake kisha akamchukua kwakua yeye alikua kwenye nafasi nzuri na kumuoa kabisa huku akiacha machungu kwa msela wake ambaye alikua ameotea mtoto mkali kipindi icho.

Wakati KDB anapambana na kipaji chake Chelsea na uongozi wake waliona Kevin De Bruyne hana kiwango Cha kucheza kwenye klabu yao.

Mwamba alipa pigo baya sana kwenye maisha yake ambalo alishawai kusema kua ilimuumiza sana aliondokewa na mwanamke anaempenda na kwenda kwa rafiki ake ambaye yeye kipindi hicho alikua na maisha mazuri akiwa amesajiliwa na Atletco De Madrid anakula mshahara mzuri huku Kevin akiwa bado anasota na maisha baada ya Jose Mourinho kumkataa kua hana kiwango cha kuanza wa kucheza kwenye timu yake.

Kutokana na mapito aliokua anapitia Kevin mwanamke huyo mrembo kabisa aliamini kuwa moja kwa moja Thibaut ndiye mwanaume sahihi kwenye maisha yake kuliko Kevin aliekua anahangaika na maisha kwa wakati huo.

Kumbuka Kevin De Bruyne alikua na urafiki na Thibaut tangu wakiwa kwenye timu Yao ya nyumbani ya kurea vipaji KRC Genk walifanya mengi walisaidia mengi na mwisho mwamba akamuibia mwanamke na maneno mengi ya kejeli.

Golikipa Courtois alionekana kuanza kupata maisha mazuri mapema baada ya yeye kusajiliwa Atletco Madrid mwaka 2011 huku KDB akiwa bado anahangaika pale darajani.

Kutokana na pigo hilo ambalo lilimyumbisha akili na kumfanya kukosa amani kabisa kutokana na upendo aliokua nao kwa bidada huyo na msaada aliokua akimpatia wakati Kevin hana kitu. Changanya na maneno ya baadhi ya viongozi wa Chelsea waliosema kua Kevin hana kipaji hivyo watamuuza hastahili kucheza Chelsea.

Kevin alipitia kipindi kigumu sana kwenye maisha yake kwani mwanamke aliekua anamsaidia mwazo pesa kidogo ameibiwa rafiki ake ambaye angemsaidia hata kidogo nae alimsaliti kisa mwanamke. Kiufupi Kevin alikua na wakati mgumu sana akiangalia maisha ya nyumbani kwao ni magumu sana.

KDB alipelekwa kwa mkopo na Chelsea huko Genk baadaye wakamuuza kwenda Weeder Bremen ya Ujerumani kwa Euro 450,000 wakati wao wakiwa walimnunua kwa Euro milioni 8 kutoka Genk.

Maisha ya mwamba yaliendelea kua magumu sana huko Ujerumani kwani kocha wa kipindi hiko wa Werder Bremen alionekana kuukosoa usajili wa kiungo huyo na kusema kua hana kiwango hivyo hawezi kumpatia nafasi.

Mwamba alikua anajitahidi kujituma lakini kocha aligoma kabisa kukubali uwezo wa Kevin De Bruyne. Alikaa benchi sana mpaka mkataba wake unamalizika, tayari ameporwa mchumba home kwao, maisha ni magumu sana.

Kutokana na ugumu wa maisha ya wazazi wa KDB, mama yake alimshawishi mwanawe aende kuishi kwa kaka ake ambaye ni mjomba wake ili aendeleze kipaji chake kwani mama ake aliamini mwanawe anakipaji cha soka kikubwa anko wake alimtia moyo sana alimwambia mda utafika mambo yatabadilika.

Kevin De Bruyne akiwa Werder Bremen na mkataba ukiwa umeisha uongozi uligoma kumuongeza mkataba wakimtaka atafute sehemu nyingine ya kwenda.

C.E.O wa Chelsea kipindi hicho mwanadada Marina aliamru Kevin De Bruyne arejeshwe Chelsea na apewe nafasi acheze, kweli bana mwamba akarejea darajani lakini mambo yalikua yale yale, kubaguliwa pamoja na uarubino alionao alikua akiishi maisha mabaya na ya uchungu sana pale Chelsea.

Mnamo mwaka 2014 kocha alieitwa mwendawazimu na asiejua kuona vipaji wa klabu yenye mashabiki wengi watukutu Wolfsburg walitoa kitita cha Euro Million 22 wakamsajili Kevin De Bruyne kutokea Chelsea na alipofika Ujerumani kocha wa Wolfsburg alimwambia 'Kevin achana na kila kitu sahau kila kitu huu ni muda wako wa kuonyesha kipaji chako na uwezo wako dunia ikufahamu cheza soka'.

Kocha alianza kumtumia kama kiungo mchezeshaji na mwamba alianza kujituma na kocha alimpa nafasi mwanzo mwisho na Maisha ya Kevin yalianza kubadilika akiwa huko.

Kutokana na moto aliouwasha na machungu ya mwanamke wake alienwambia kua yeye sio romantic wara hana dalili za kufanikiwa na akamkimbia na kwenda kwa rafiki ake mwamba alikua anacheza mpaka anabadilika rangi anakua mwekundu.

Mwaka 2015 basi hapo mda ukaamua na kusema ukweli kua nani Bora nani anapanga maisha ya watu Manchester City, The Citizen walimsajili Kevin De Bruyne kwa kitita Cha Euro Million 76 kutoka kwa wahuni wa ujeruman Wolfsburg na hapo ndipo maisha ya KDB yalipoanza kubadilika.

Mwamba alioa mwanamke mwingine mrembo ambaye hivi sasa amemzalia watoto wazuri na warembo mwamba amebadilisha maisha ya nyumbani kwao na mwamba arimjengea Jumba la kifahari mjomba wake huko Belgium.

Yule bidada aliemkimbia kwakuona kua mwamba hawezi kufanikiwa kutokana na mapito ya Dunia nafikiri moyoni hua anakili kua mwamba ningemvumilia kidogo mambo yangejipa kwani Kevin anacheza nafasi ya kiungo uwanjani huku bwana ake akicheza nafasi ya golikipa kwenye klabu ya Real Madrid Kdb analipwa mshahara mara 6 ya mshahara anaolipwa Courtois na Kevin kwa sasa ndiye mfalme pale Manchester City na mashabiki wa Manchester City wanamuita The Manchester City wakimanisha kua yeye Kevin ndiye Manchester City kwani mafanikio mengi walioyapata City yamepitia kwenye mikono yake.

Kevin De Bruyne anapokea kiasi cha Euro 400,000 kila mwezi kwenye klabu yake ya Manchester City na ndiye mchezaji mwenye assists nyingi kuliko mchezaji yoyote yule tangu City ianzishwe.

Kutokana na dharau walizowahi kumuonyesha Chelsea kama unafuatiria vizuri mechi za Manchester City na Chelsea kama Kevin yumo basi hua hana huruma kabisa hupiga mashuti makali Sana na hujituma mara dufu zaidi.

Pia Wakati Real Madrid wanaiondoa Manchester City michuano ya UEFA Champions League mwaka 2021/22 Mwamba aliumia sana kitendo ambacho kilipelekea yeye kushindwa kupata usingizi siku hiyo bahati nzuri msimu uliopita Real Madrid wakapangwa mtoano na Manchester City Tena unaambiwa Kevin alikua akicheza kwa tahadhali kubwa mechi za ligi ili asiumie akutane na Real Madrid.

Mashabiki waliokua karibu na lango walisema Kevin alikua akipiga mashuti makali sana mara 3 ya yale anayopiga Kila alipokua akikalibia lango la Real Madrid na wengi walitafsiri kua huenda anafanya hivyo kumuonyesha mwanamke wake aliyemkimbia kua yeye hawezi kufanikiwa kama ulicheck game ya City na Madrid ile Madrid anakufa goli nne utaelewa nachokwambia mwamba alikua anakamia sana.

Kevin De Bruyne hua haipendi Chelsea Toka moyoni kwani anaamini yeye alikua na uwezo wa kuichezea Chelsea ila wao walimkatisha tamaaa na kumtenga sana hivyo anaamini Chelsea walihusika zaidi kwenye maumivu yake aliopitia pia hajawahi kua na maelewano na rafiki ake wa zamani hata wakiwa nation Team

Kevin hana story naye japo Courtois hua anajitahidi lakini mwamba hua hataki shobo kabisa wara hua hataki salamu yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live