Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kevin Sowax afuta picha zote za Mobetto

Sowax Mobetto.png Kevin Sowax afuta picha zote za Mobetto

Wed, 7 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mfanyabiashara Kevin Ahyi-sena maarufu kama Kevin Sowax ambaye ni raia wa Togo amefuta picha zake zote alizopiga na mrembo Hamisa Mobeto kwenye akaunti yake ya Instagram.

Ikumbukwe Hamisa alikuwa akimpost Kevin akisema ni mpenzi wake na mwaka jana (2023) Kevin alikuja Tanzania akidai kuwa amekuja kibishara pamoja na kuenjoy na mpenzi wake huyo ambaye pia ni mzazi mwenzake na fdiamond Platnumz.

Wakati hayo yakijiri, Harmonize alionekana kunyemele penzi la Hamisa Mobetto na alishindwa kabisa kuficha hisia zake, jambo ambalo lilimlazimi Mmakonde kumueka kwenye Wallpaper yake ya simu.

Harmonize kumueka Mobetto wallpaper haikutosha, alimuimbia wimbo wa Side Nigar "Don't you see your beautiful face in my wallpaper" ukiwa mstari mmoja wa wimbo huo.

Baada ya kuona hakuna dalili za kukubaliwa, Harmonize baadaye aliamua kwenda kwa Poshy Queen.

Ni wiki chache tu baada ya Kevin kusherehekea birthday yake, ameamua kuzifuta picha zote akiwa na Hamisa huku chanzo cha maamuzi hayo kikiwa hakijaelewa iwapo waneachana ama kuna jambo jingine.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live