Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya Ubakaji: Mwanasheria wa Chris Brown ajitoa

Attachment Chris Brown Chris Brown

Fri, 11 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanasheria wa kesi ya ubakaji ambayo inamkabili mwimbaji maarufu wa muziki duniani, Chris Brown ametangaza kujitoa kwenye shauri hilo.

Ariel Mitchell amesema amejitoa kufuatia ushahidi wa sauti (voice note) pamoja na ujumbe mfupi ambazo jana CB alizianika hadharani zikionesha hakuwa na hatia.

Ushahidi uliotolewa na Breezy ulimuanika wazi mwanamke huyo kuwa ndiye alikuwa akimuhitaji mwimbaji huyo wa R&B tofauti na madai yake. Mwanasheria huyo amesema mteja wake hakumueleza ukweli kabla kwani angelifuta.

Chris Brown ameendelea kudai aombwe msamaha hadharani, lakini pia ameendelea kuvitaka vyombo habari kuripoti habari hii kama ambavyo waliripoti tuhuma zake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live