Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya Mwijaku na Nandy yaunguruma Mahakamani leo

MWIJAKU NA NANDYY Kesi ya Mwijaku na Nandy yaunguruma

Fri, 12 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Leo Ijumaa Agosti 12, 2022, kesi inayomkabili msanii wa Bongo Fleva, Faustina Charles Mfinanga almaarufu Nandy imeunguruma kwa mara nyingine katika Mahakama ya Mwanzo ya Sinza jijini Dar.

Kesi hiyo ambayo imefunguliwa na Mtangazaji wa Clouds FM, Burton Mwambe almaarufu Mwijaku kwa madai kuwa alitumiwa vibaya na Nandy bila makubaliano yake.

Mwijaku ameieleza mahakama kuwa, walielewana na Nandy afanye tangazo kwa ajili ya Nandy Festival ambapo tangazo hilo lilifanyika hospitalini na baada ya tangazo kukamilika Nandy alilikataa tangazo hilo ila baada ya muda alikuta Nandy ameliposti na wakashindwa kuelewa hivyo akaaumua kwenda mahakamani.

Kesi hiyo ilisikilizwa kwa mara ya kwanza Agosti 9-8, 2022 na ilipigwa tarehe mpaka leo tarehe 12-8-2022, baada ya Mwijaku kufika na wakili wake pia Nandy kuwakilishwa na meneja wake pamoja na wakili imepigwa tarehe tena mpaka tarehe 19-8-2022 hapohapo Mahakama ya Mwanzo Sinza.

Hakimu ameomba wahusika yaani mshitaki na mshitakiwa waje na nyaraka stahiki ikiwemo mkataba waliosaini kwa ajili ya tangazo hilo, endapo mmojawao ataonekana ameenda kinyume na mkataba ule, basi atamlipa mwenzake na madai ya Mwijaku ni kwamba anamdai Nandy shilingi milioni 10.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live