Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Kerry afahamu anayeishi naye si baba yake mzazi akiwa na miaka 41

Kerryb2d Kerry afahamu anayeishi naye si baba yake mzazi akiwa na miaka 41

Tue, 26 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muigizaji Kerry Washington mwenye umri wa miaka 46 afunguka kufahamu ukubwani kuwa baba anayeishi naye siyo baba yake mzazi.

Kerry amedai kuwa aligundua hilo mwaka 2018 baada ya kuwashirikisha wazazi wake kuwa amepanga kuonekana kwenye Tv show ya “Finding Your Roots” ya Henry Louis Gates Jr ambayo watu mashuhuri hujifunza kuhusu mababu zao kwa kupima DNA.

Baada ya kuwashirikisha hilo ndipo wazazi wake walimualika nyumbani na kumueleza ukweli kuwa alikuwa ni mtoto aliyepatikana kwa upandikizwaji wa mbegu za mwanaume mwingine, baada ya wazazi hao kutafuta mtoto kwa njia ya kawaida bila mafanikio.

Hata hivyo Kerry amedai kuwa jina la mtu aliyetoa mbegu zake halikufahamika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live