Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kendrick Lamar kulibariki jukwaa la Supee Bowl 2025

Skysports Kendrick Lamar Super Bowl 6679847 Kendrick Lamar kulibariki jukwaa la Supee Bowl 2025

Tue, 10 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa muziki kutoka Marekani Kendrick Lamar ameteuliwa rasmi kuwa msanii atakayeongoza shoo ya Halftime kwenye Super Bowl ya mwaka 2025. Habari hizi zimethibitishwa na waandaaji wa tukio hilo kubwa la michezo na burudani.

Shoo ya Halftime ya mchezo wa kila mwaka wa ubingwa wa ligi ya Kitaifa ya Soka ya Merika Super Bowl inajulikana kwa kuvutia watazamaji wa kimataifa, na Kendrick Lamar atakuwa msanii mwingine kuungana na orodha ya mastaa wakubwa waliowahi kuongoza tukio hilo.

Wasanii waliowahi kufanya shoo ya Halftime kwenye mashindano hayo ni mrembo Rihanna mwaka 2023 alipotoa burudani ya kipekee iliyojaa nyimbo zake maarufu kama "Umbrella" na "Diamonds." Msanii mwingine ni Usher Raymond mwaka 2023.

Rapa huyo anajulikana kwa nyimbo zake zenye mafanikio kama "HUMBLE." na "Alright," anatarajiwa kutoa shoo ya kusisimua ambao itakumbukwa kwa muda mrefu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live